MCA wa Kiambu Ezra Kabuga afariki katika ajali

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwakilishi wadi mteule wa kaunti ya Kiambu Ezra Kabuga Kihara amefariki mapema Jumapili kwenye ajali ya barabarani eneo la Juja, katika barabara ya Thika.

Marehemu ambaye ni wakili aliaga dunia baada ya gari lake aina ya Subaru Forester lilipoingia ndani ya lori kutoka nyuma.

MCA huyo alifariki papo hapo kwenye ajali hiyo ambayo video ya ajali ilionyesha kuwa gari hilo lilishika moto baada ya kugonga lori.

Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya Montezuma kusubiri upasuaji huku magari yote mawili, yakibebwa hadi katika kituo cha polisi kilicho karibu.

Website |  + posts
Share This Article