Mbweha wa Algeria waponea chupuchupu AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa AFCON mwaka 2019 Algeria ukipenda The Foxes wametoka nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya mabao 2 dhidi ya Burkina Faso, katika mchuano wa kundi  D uliosakatwa Jumamosi jioni mjini Bouke nchini Ivory Coast.

Mohamed Konate alipachika bao la kwanza kwa Burkina Faso ukipenda The Stallions, kunako kipindi cha kwanza kabla ya Algeria kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Baghdad Bounedjah mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Burkinabe ilirejea uongozini  kupitia kwa penati ya Betrand Traore, lakini Bounedjah akasawazisha tena dakiak ya mwisho ya muda wa mazidadi.

Algeria wana pointi 2 huku Burkina Faso wakisalia uongozini kwa alama 4.

Share This Article