Mbunge wa zamani wa eneo bunge la Baringo Kaskazini Willy Kamuren amefariki.
Familia yake imethibitisha kuwa mbunge huyo alifariki wakati akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi.
Kamuren alikuwa mbunge wa eneo hilo kati ya mwaka 1963 hadi 1969.
Aliliwakilisha eneo bunge la Baringo Kaskazini kwa tiketi ya chama cha KADU.
Kisha baadaye aliteuliwa kwenye bunge kati ya mwaka wa 1983 kabla ya kuchaguliwa tena kuliwakilisha eneo bunge hilo kati ya mwaka 1988 hadi 1997.
Aidha, aliwahi kuhudumu kama Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais.
Kifo chake kinakuja wakati wakazi wa kaunti ya Baringo wanaomboleza kifo cha Seneta William Cheptumo.