Mbunge wa Kitui Mashariki Nimrod Mbai aachiliwa kwa dhamana

Tom Mathinji
1 Min Read

Mbunge wa Kitui Mashariki Nimrod Mbai ameachiliwa kutoka kituo cha polisi cha Kitengela kwa dhamana ya shilingi 50,000 pesa taslimu. 

Hii ni baada ya mbunge huyo kujisalimisha katika kituo hicho Jumatano asubuhi, baada ya kumdhulumu afisa wa kampuni ya umeme nchini, KPLC Jumatatu wiki hii.

Maafisa wa polisi walitwaa bastola yake kabla ya kumwachilia huru.

Mzozo ulizuka wakati maafisa wa kampuni ya KPLC walifika nyumbani kwa mbunge huyo kukata umeme ambao kwa mujibu wa maafisa hao uliunganishwa kinyume cha sheria.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *