Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno afariki kwa ajali ya helikopta

Tom Mathinji
1 Min Read

Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno amethibitishwa kuwa miongoni mwa watu sita waliofariki baada ya helikopta kuanguka katika eneo bunge la Mosop kaunti ya Nandi Jumamosi alasiri.

Kifo cha Ng’eno kimethibitishwa na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula kupitia kwa taarifa.

“Ni Kwa huzuni kubwa nafahamisha Bunge la Taifa kuhusu kifo cha ghafla mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno,” alisema kwa Spika Wetang’ula.

Huku akituma rambirambi Kwa familia na marafiki wa Ng’eno, Wetang’ula alimtaja mbunge huyo kuwa aliyejitolea kuwahudumia wananchi kwa ujasiri.

“Kwa niaba ya Bunge la Taifa, Huduma ya kuwaajiri wafanyakazi wa Bunge na kwa niaba yangu, tunatuma rambirambi Kwa familia, jamaa na marafiki wa mheshimiwa Johana Ng’eno,” aliongeza Spika huyo.

Aidha Wetang’ula alibuni kamati itakayoshirikiana na familia kuandaa mazishi ya mbunge huyo.

Kamati hiyo itaongozwa na mbunge wa Tinderet Julius Melly akisaidiwa na mbunge Mugambi Rindikiri pamoja na wanachama wengine wanane.

Mbunge huyo pamoja na washirika wake walikuwa kwenye ndege hiyo ilipoanguka leo jioni.

Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo, Samuel Mukuusi alithibitisha kisa hicho kilichotokea mwendo wa saa kumi na dakika 45.

Share This Article