Mbunge Mugirango Kusini Silvanus Osoro amekanusha madai ya kutoa hongo katika hafla moja iliyoandaliwa kaunti ya Bomet.
Osoro ambaye alihojiwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC jana Jumatatu amesema kuwa kamwe hakumhonga yeyote na badala yake anaitaka tume hiyo itoe ushahidi kuthibitisha madai hayo.
Katika mkutano wa Bomet, Osoro alinukuliwa akisema baadhi ya wabunge hutoa hongo ili kupata safari za ughaibuni.
Osoro ambaye pia ni kiranja wa walio wengi katika bunge la kitaifa, alitoa matamshi hayo kwenye mkutano ulioandaliwa Oktoba 29 na mwakilishi wa kina mama wa kaunti ya Bomet Linet Chepkorir almaarufu Toto.