Mbunge Njeri Maina aandikisha taarifa kwa polisi

Tom Mathinji
1 Min Read

Mwakilishi wanawake wa kaunti ya Kirinyaga Njeri Maina ambaye alishambuliwa na wahuni na kupata majeraha ya kichwa, ameandikiaha taarifa kwa maafisa wa upelelezi wa makosa ya jina DCI katika kaunti ya Kirinyaga.

Mbunge huyo ambaye alilazwa katika Nairobi hospital tangu kutoka kwa shambulizi hilo Jumanne tarehe  22 mwezi Agosti, aliwasili katika afisi za DCI akiwa kwa kiti cha magurudumu akiwa ameandamana na wakili wake pamoja na mbunge wa Rarieda Otiende Omollo.

Njeri alishambuliwa baada ya mkutano aliokuwa akihudhuria kugeuka na kuwa ghasia.

Akizungumza muda mfupi baada ya tukio hilo, mbunge huyo alisema alishambuliwa alipokuwa Akizungumza na wakazi mjini Kerugoya, wakati  kundi la wahuni lilijaribu kumzuia kuwahutubia wakazi.

“Ni watu ninaowajua, nimevuja damu lakini nitawatetea watu wa kaunti ya Kirinyaga. Nimechaguliwa katika kaunti hii ya Kirinyaga na lazima watu wa kaunti hii wapate haki yao,” alisema mbunge hiyo.

Mbunge huyo aliyekuwa ameandamana na Mwakilishi wadi ya Baragwi David Mathenge, alipelekwa katika hospitali ya Kerugoya alikotibiwa kabla ya kuhamishwa hadi Nairobi Hospital.

Wakazi na wabunge wamekashifu vikali shambulizi hilo.

Share This Article