Mbunge wa Emurua Dikirr Johana Ng’eno atazikwa siku ya Ijumaa, Machi 6 mwaka huu katika kaunti ya Narok.
Ng’eno alifariki pamoja na watu wengine watano kwenye ajali ya helikopta iliyotokea katika eneo la Mosop, Nandi.
Waathiriwa wote sita wa ajali hiyo wataandaliwa ibada ya mazishi ya pamoja tarehe ambayo itatangazwa baadaye.
Nyumbani kwa mbunge huyo mtaani Karen, viongozi mbalimbali waliwasili, moja baada ya mwingine, kuifariji familia ya marehemu.
Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi waliowasili nyumbani kwa mbunge huyo ambaye alikuwa akihudumu muhula wake wa tatu hadi mauti yalipomfika.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini, KCAA imeanzisha uchunguzi kuhusu kilichosababisha ajali hiyo.
Ndege hiyo ilianguka katika lokesheni ndogo ya Kabiyet, eneo bunge la Mosop juzi Jumamosi jioni.
Viongozi mbalimbali wamemsifia marehemu Ng’eno wamkimtaja kuwa mchapa kazi aliyetumikia taifa na wakazi wa eneo bunge la Emurua Dikirr kwa uadilifu.