Mbunge Innocent Obiri aondolewa mashtaka ya uchochezi

Tom Mathinji
1 Min Read

Mahakama moja ya Kisii, imemuondolea lawama mbunge wa  Bobasi Innocent Obiri dhidi ya uchochezi na uharibufu wa Mali yanayodaiwa kutekelezwa miaka tano iliyopita.

Hakimu mkuu Nathan Lutha, pia alimwachilia huru mlinzi wa mbunge huyo konstabo wa polisi Charles Nyakweba kutokana na makosa hayo.

Akiitoa hukumu hiyo hakimu huyo mkuu alidokeza kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya wawili hao, yanayosemekana yalitekelezwa katika timbo moja la kibinafsi katika eneo bunge la Nyamonema.

Mwenye timbo hilo alidai kuwa wawili hao waliwachochea wakazi kuharibu Mali ya kampuni yake na kuhujumu Operesheni zake.

Wakili wa mbunge huyo Katwa Kigeni, alisema madai hayo hayakuwa ya kweli, huku akipongeza mahakama kwa kuwaachilia huru wawili hao.

Akizungumza baada ya kutupiliwa mbali kwa mashtaka hayo, Obiri alisema alikuwa amefika katika timbo hilo kulalamikia madhara yanayotokana na timbo hilo kwa wakazi.

Baadhi ya madhara hayo ni maafa yanayotokana na matatizo ya kupumua.

Share This Article