Wizara ya Kilimo imepuuzilia mbali madai kwamba shehena ya mbolea ya msaada kutoka kwa serikali ya Urusi imetoweka.
Katika taarifa kupitia Halmashauri ya Nafaka na Mazao nchini, NCPB, wizara hiyo imesema usafirishaji wa shehena hiyo ulikabidhiwa NCPB ambayo imejukumiwa kupokea na kusambaza mbolea.
“Kiwango kilichotolewa ni tani metric 34,400. Hata hivyo, baada ya meli kutia nanga, kiwango kilichopokelewa ni tani metric 33,835,” ilisema NCPB.
Ripoti zilidai kuwa tani 564 za mbolea hiyo ya msaada kutoka Urusi zilitoweka ikiwa safarini.
Kulingana na NCPB, kiwango cha mbolea hiyo kinawakilisha asilimia 98.36 dhidi ya kiwango kilichonakiliwa katika shehena hiyo.
Wiara hiyo ilisema mbolea hiyo ilitolewa kwa misingi kwamba itawasilishwa bandarini, na kwamba serikali haikugharimia usafirishaji wake.