Mkondo wa tano wa mbio za nyika nchini utaandaliwa Jumamosi Disemba 14 mjini Olkalou huku zaidi ya washiriki 500.
Mbio hizo zitaandaliwa katika uwanja wa Olkalou Arboretum,yakiwa mashindano ya tano tangu mkondo wa nne uliofanyika kaunti ya Bomet Novemba 30.
Ilivyo desturi mkondo huo utashirikisha vitengo vya chipukizi chini ya umri wa miaka 20 kwa wanaume kilomita 8, na kilomita 6 kwa wasichana ,kilomita 10 kwa wanaume na wanawake na mzunguko wa kilomita mbili.
Washindi wa kilomita 10 watatuzwa shilingi 50,000 nafasi ya pili 40,000 na shilingi 20,000 kwa watakaomaliza nafasi ya tatu.