Msimu mpya wa mashindano ya riadha uantarajiwa kung’oa nanga Oktoba 19, kwa mbio za nyika za Iten kaunti ya Elgeyo Marakwet, kabla ya kuelekea kaunti ya Machakos Novemba 2 kwa musururu wa pili.
Kaunti ya Bomet itaandaa msururu wa tatu tarehe 30 Novemba huku ule wa nne ukifanyika Olkalou Disemba 14, na kumalizikia kaunti ya Kisii Januari 4 mwakani.
Mbio za kitaifa za nyika zitaadaliwa Februari 8 mjini Ruiru, kabla ya mbio za Sirikwa Classic World Cross Country Tour tarehe 23, eneo la Lobo Village mjini Eldoret.
Mkondo wa kwanza wa mbio za uwanjani ukipenda Track and Field/Relay Series utaanzia Bukhungu kaunti ya Kakamega baina ya Februari 13 na 15 mwaka ujao.
Mashindnao ya Dunia wa ndani ya ukumbi maarufu kama World Athletics Indoor yataandaliwa kati ya Machi 21 na 23 mwaka ujao mjini Nanjing, China.
Makala ya tano ya mashindano ya Kip Keino Classic,yataandaliwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani Mei 31 mwakani.
Majaribio ya kitaifa kwa mashindano ya Dunia yaandaliwa Juni na Julai mwaka ujao, huku mashindano hayo yakiandaliwa mjini Tokyo,Japan kati ya Septemba 13-21 mwaka 2025.