Mbio za kitaifa zasukumwa mbele hadi Mei 21 na 22

Dismas Otuke
1 Min Read

Mashindano ya kitaifa ya riadha ambayo pia yangetumika kama majarbio ya kuteua kikosi cha Kenya kwa mashindano ya Afika yamesongezwa mbele kutoka Mei 16 -18 katika uwanja wa Nyayo, hadi tarehe 21 na 22 mwezi huu katika uwanja wa Ulinzi Sports Comlex.

Chama cha riadha Kenya kitatumia mashindano hayo kuteua timu ya kenya itakayoshiriki makala ya 23 ya mashindano ya bara Afrika yatakatoandaliwa mjini Douala Cameroon, baina ya tarehe 15 na 22 mwezi ujao.

Kenya italenga kuhifadhi taji ya jumla iliyonyakua mwaka 202 nchini Mauritius kwa dhahabu 10,fedha 5 na shaba 8.

Share This Article