Mbinu mpya za kukabiliana na wizi wa mitihani zatangazwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Watakaojihusisha na wizi wa mitihani, mashakani.

Huku mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE ukiingia wiki ya nne leo Jumatatu, waziri wa elimu Julius Migos, ameelezea mbinu mpya za kukabiliana na wizi wa mitihani.

Akizungumza baada ya kuongoza zoezi la kusambaza mitihani katika kaunti ndogo ya Lang’ata Jijini Nairobi, waziri huyo alisema watakaojihusisha na udanganyifu huo watachukuliwa hatua binafsi na wala sio kituo chote cha mtihani.

Migos alionya kuwa mwanafunzi yeyote aktakayepatikana akishiriki wizi wa mitihani, atachukuliwa hatua binafsi.

“Mwaka huu hatutachukulia hatua shule nzima hatua, lakini mtu binafsi atakayeshiriki wizi wa mitihani,” alisema waziri huyo.

“Ikiwa mwanafunzi atapenyeza rununu katika kituo cha mtihani, tutajua ni mwanafunzi huyo kwa kuwa kila karatasi ya mtihani ina bambari spesheli ya kila mwanafunzi. Mwanafunzi huyo atachukuliwa hatua matokeo yatakapotolewa,” aliongeza Migos.

Wakati huo huo, waziri huyo alitoa wito kwa idara ya mahakama kuhakikisha wanaohusika katika wizi wa mitihani wanachukuliwa hatua za kisheria.

Share This Article