Mbai apendekeza ugavi wa raslimali kwa kuzingatia ukubwa wa eneo

Dismas Otuke
2 Min Read

Mbunge wa Kitui East Nimrod Mbai amependekeza mfumo mpya wa ugavi wa raslimali kwa kuzingatia ukubwa wa eneo maarufu kama One Man, One Kilometre,One Shilling .

Mbai anayewania Uenyekiti wa chama cha United Democratic Alliance(UDA),amepinga mfumo unaopendezwa na naibu Rais Rigathi Gachagua, wa one man,one vote one shilling akitaka ukubwa wa eneo kuzingatiwa pia.

“Tunapinga kabisa mfumo huu wa one man, one shilling formula,” akasema Mbai. “Inatakiwa iwe one man, one kilometre, one shilling.”

Kulingana na Mbai kaunti ya Kitui ina idadi ya watu waliotapakaa na endapo mfumo unaopendekezwa na naibu Rais utaidhinishwa  ,wakazi wa Kitui wataathirika pakubwa ikilinganishwa na maeneo kama ya Mlima Kenya.

Mbunge huyo anayehudumu kwa muhula wa pili afisini amesema atajiunga na wabunge wa kutoka maeneo kame kama ya kazkazini mashariki mwa nchi na pwani kupinga mfumo huo wa ugavi.

“Mfumo huu unalenga kugawanisha nchi na unapaswa kupingwa vikali,”akasema Mbai. “Tunataka mfumo ambao unazingatia ukubwa wa eneo ambao utawezesha Gavana wetu wa Kitui kupata shilingi bilioni 8 zaidi.”

Mbai amesisitiza kuwa iwapo ukubwa wa eneo utazingatiwa katika ugavi wa raslimali za kitaifa ,kaunti ya Kitui itapata shilingi milioni 300 kutoka milioni 150 inazopata kwa sasa.

Mbai alisema haya katika kaunti ya Kitui baada ya kukutana na viongozi wa mashinani wa chama cha UDA, kabla ya uchaguzi ulioratibiwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi huu ambapo ametanagza azma ya kuwania uenyekiti.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *