Baraza la Mawaziri limeidhinisha sheria itakayowaadhibu vikali maafisa wa serikali watakaozuia kuapishwa kwa Rais baada ya uchaguzi mkuu.
Kulingana na adhabu hiyo, watakaojaribu kuzuia kuapishwa kwa Rais watatozwa faini ya shilingi milioni moja au kufungwa gerezani kwa kipindi cha miaka kumi.
Sheria hiyo ilikuwa imependekezwa katika muswada wa mwaka 2024, kuhusu kuingia afisini kwa Rais baada ya uchaguzi mkuu.
Sheria hiyo itashuhudia ubadilishanaji wa mamlaka kwa njia isiyo na tashwishi baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
Muswada huo sasa utawasilishwa bungeni kujadiliwa na kupitishwa au kukataliwa.
Baadhi ya mapendekezo mengine katika muswada huo ni ulinzi kamili wa Rais na Naibu Rais Mteule sawia na Rais aliye mamlakani.
Mabadiliko mengine yanapendekeza ukabidhi wa mamlaka hata bila kuwepo kwa Rais anayeondoka kwa Rais mteule.