Mipango ya ziara ya Rais Ruto eneo la Nyanza yashika kasi

Martin Mwanje
1 Min Read

Mawaziri Eliud Owalo wa Habari na Mawasiliano na Kipchumba Murkomen wa Barabara leo Ijumaa wamekutana na wabunge watano wa eneo la Nyanza. 

Wabunge hao ni pamoja na Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o wa Langata, Elisha Odhiambo wa Gem na Caroli Omondi wa Suba Kusini.

Owalo anasema mkutano kati yao ulinuia kupanga ziara ijayo ya Rais William Ruto katika eneo la Nyanza.

“Mambo makuu tuliyoangazia wakati wa majadiliano yetu ni barabara na miundombinu mingine katika eneo la Nyanza,” alisema Waziri Owalo.

Wabunge hao ikiwa ni pamoja Seneta wa Kisumu Prof. Tom Ojienda na wabunge Gideon Ochanda (Bondo) Caroli Omondi (Suba Kusini), Elisha Odhiambo (Gem), Mark Nyamita (Uriri), Paul Abuor (Rongo) na Jalang’o Julai 4 walikutana na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.

Ingawa ni wanachama wa ODM, wameapa kufanya kazi na utawala wa Kenya Kwanza kukuza maendeleo katika maeneo yao baada ya tofauti kuchipuka kati yao na chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga.

 

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *