Mawaziri 5 wa zamani wapoteza nyadhifa zao

Martin Mwanje
1 Min Read

Jumla ya mawaziri watano wa zamani wamepoteza nyadhifa zao baada ya kuteuliwa kwa mawaziri wapya kuhudumu katika nyadhifa zao. 

Sasa ni rasmi kwamba Susan Wafula Nakhumicha hatahudumu tena kama Waziri wa Afya baada ya Dkt. Debra Mlongo Barasa kuteuliwa katika wadhifa huo.

Kipchumba Murkomen pia amepoteza wadhifa wake baada ya Davis Chirchir kuteuliwa kuwa Waziri wa Barabara na Uchukuzi.

Kadhalika, Ezekiel Machogu hana bahati baada ya Julius Migos Ogamba kuteuliwa kama Waziri wa Elimu.

Mwingine aliyepoteza wadhifa wake ni Eliud Owalo ambaye awali alihudumu kama Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali. Rais Ruto amemteua Margaret Nyambura Ndung’u kushikilia wadhifa huo.

Eric Muriithi Muuga ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Maji ikiwa na maana kuwa Zachariah Njeru amepoteza wadhifa huo.

Mwingine ambaye chuma chake ki motoni ni Mwanasheria Mkuu Justin Muturi ambaye wadhifa wake umekabidhiwa Rebecca Miano ambaye awali alihudumu kama Waziri wa Biashara.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *