Washiriki kutoka nchi 28 barani Afrika walikongamana katika Chuo Kikuu cha Chuka kujadili mbinu za kukabiliana na ukosefu wa chakula, hasa kwa kutumia tekonolojia za jeni katika sekta ya kilimo.
Wametaja hatua hiyo kuwa muhimu kwa sababu idadi ya watu inayoongezeka barani humo inasababisha ongezeko la mahitaji ya chakula kila mwaka.
Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Makamu Chansela wa Chuo Kikuu cha Chuka Prof. Henley Mutembei alisema matumizi ya teknolojia za jeni yatatekeleza jukumu muhimu katika kuimarisha uchumi wa Afrika kwa kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza utegemezi kwa masoko ya kimataifa.
Aliongeza kuwa Afrika ina uwezo wa kujitosheleza kwa chakula ikiwa itakumbatia uvumbuzi na teknolojia katika sekta ya kilimo.
Taarifa ya Daniel Njoka