Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ametuma risala zake za rambi rambi kwa familia zilizopoteza jamaa zao kwenye mkasa wa mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa nchini. Kulingana na ujumbe wake uliotumwa kwa vyombo vya habari, Kenyatta amesikitia watu waliofiwa, kuharibiwa mali na pia kupoteza makao.
Aidha Kenyatta ametoa wito wa kuungana pamoja kama taifa ili kuwafaa waliolemewa na hali hii. Kiongozi huyo alitoa mchango wake binafsi wa shilingi 2M kwa shirika la msalaba mwekundu ili kuendeleza juhudi za kuwasaidia walioathirika.
https://art19.com/shows/matukio-ya-taifa/episodes/9be4ae9a-c10b-43d0-8696-ff62366c97e4