Matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne, KCSE yatatangazwa mwezi ujao na wala sio mwezi huu ilivyotarajiwa.
Usahihishaji wa mtihani huo ulimalizika wiki hii.
Yamkini matokeo hayo yamecheleweshwa ili kuhakiki vyema na kuepusha kasoro kama zilizoshuhudiwa katika matokeo ya mwaka uliopita.
Wanafunzi 965,501 walikalia mtihani wa KCSE mwaka huu.