Matokeo ya kura za urais yaashiria Namibia itampata Rais wa kwanza mwanamke

Ili kutangazwa Rais mshindi wa Urais mshindi anapaswa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote.

Dismas Otuke
1 Min Read

Matokeo ya mwanzo ya kura za urais zilizopigwa wiki jana nchini Namibia, yanaashiria kuwa taifa hilo litampta Rais wa kwanza mwanamke.

Kwenye matokeo ya awali, Makamu wa Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah wa chama tawala cha SWAPO, anaongoza kwa asilimia 54.82 ya kura baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 65.57 ya kura zote kufikia mapema leo Jumanne.

Ili kutangazwa Rais, mshindi wa urais anapaswa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote.

Uchaguzi wa urais uliandaliwa Novemba 27 lakini upigaji kura ukaongezwa muda hadi Novemba 30 katika baadhi ya maeneo, baada ya wapigaji kura wengi kushindwa kupiga kura kutokana na ukosefu wa vifaa vya kupigia kura na hitilafu za kimitambo.

Hata hivyo, kiongozi wa upinzani Panduleni Itula wa chama cha Independent Patriots for Change aliyepata asilimia 28 pekee ya kura tayari amekataa matokeo ya kura hizo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *