Matayarisho yamekamilika kuupokea mwili wa marehemu Raila Odinga, almaarufu Baba, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA kuanzia saa tatu unusu asubuhi ya leo.
Viongozi wakuu serikalini wakiongozwa na Rais William Ruto wanatarajiwa kuupokea mwili huo.
Majeshi ya Kenya yataongoza hafla hiyo katika uwanja wa KJIA, kabla ya mwili kusafirishwa hadi makafani ya Lee.
Zulia nyekundu limekitwa katika uwanja wa KJIA, usalama wa hali ya juu umeimarishwa tayari kwa mapokezi ya mwili wa marehemu Raila.