Matayarisho ya sherehe za ufunguzi wa Olimpiki yakamilika

Dismas Otuke
1 Min Read

Matayarisho kwa sherehe za ufunguzi wa makala ya 33 ya michezo ya Olimpiki yamekamilika huku usalama ukiimarishwa mjini Paris na kando ya mto Siene ambapo hafla hiyo itaandaliwa Ijumaa ijayo.

Wanamichezo takriban 7,000 watapiga gwaride wakitumia mashua kwa umbali wa kilomita sita mbele ya mashabiki laki tatu ,wanaotarajiwa kupiga foleni kando ya mto Siene wakati wa sherehe za ufunguzi .

Polisi wa Ufaransa wanapigwa jeki na wenzao kutoka Uhispania,Uingereza na Qatar.

Mwigo wa sherehe za ufunguzi umeandaliwa mapema leo, huku vyombo vya habari na raia wakizuiwa kuhudhuria.

Wakazi wa mji mkuu wa Paris wameathiriwa na ukosefu wa huduma muhimu kutokana na kufungwa kwa barabaraba nyingi kutoka na kuingia mjini.

Tiketi zipatazo milioni 8.7 za michezo ya Olimpiki ya mwaka huu tayari zimeuzwa, ikiwa rekodi mpya kushinda ile ya awali ya Olimpiki ya 1996 ambapo tiketi nyingi ziliuzwa.

Idadi hiyo ya tiketi inatarajiwa kuongezeka kwani bado kuna tiketi kadhaa ambazo hazijauzwa katika fani 45 za michezo inayoshirikishwa mwaka huu.

Runinga ya taifa ya KBC channel 1 itarusha mubashara michezo hiyo ambayo itaanza rasmi julai 24 na kukamilika Agostiu 11.

Website |  + posts
Share This Article