Matasi afungiwa kucheza kwa miezi mitatu na FKF

Dismas Otuke
1 Min Read

Mlinda lango wa klabu ya Kakamega Homeboyz na timu ya taifa Harambee Stars, Patrick Matasi, amepigwa marufuku ya kucheza kwa miezi mitatu na Shirikisho la Soka humu nchini – FKF.

Hii ni baada yake kutuhumiwa kuhusika katika kashfa za upangaji matokeo ya mechi katika video iliyozagaa mitandaoni jana Alhamisi.

Kulingana na waraka huo, FKF imemfungia Matasi kushiriki mechi zote zinazoendeshwa na shirikisho hilo kwa mujibu wa sheria ya 7, aya ya pili ya mwaka 2016.

Sheria hiyo imepiga marufuku upangaji matokeo ya mechi, madai anayokabiliwa nayo Matasi.

Kipa huyo aliye na umri wa miaka 37, aliichezea Harambee Stars jumla ya mechi 30.

Mara ya mwisho kwake kujumuishwa kikosini ilikuwa mwezi Oktoba mwaka jana, katika mchuano wa kufuzu Kombe la Afrika mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *