Kocha Mkuu wa Tusker FC Robert Matano ameachana na klabu hiyo yenye makao yake mtaani Ruaraka baada ya kuwafunza kwa kipindi cha miaka sita iliyopita.
Matano aliye na umri wa miaka 60 amewaongoza wagema mvinyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, mara mbili katika kipindi hicho cha miaka sita.
Kocha huyo ni mmoja wa wakufunzi walio na ufanisi mkubwa nchini Kenya,akishinda Ligi kuu mara nne akiwa na SOFAPAKA mwaa 2009 na Tusker mwaka 2020-2021 na 2021-2022.
Wakati uo huo Tusker FC imewaruhsu wachezaji 11 kuondoka baada ya kandarasi zao kukamilika .
Wanandinga hao ni pamoja na Eric Kapaito, Daniel Sakari, Brian Bwire, Eric Zakayo, Stewart Omondi, Collins Otieno, Jimmy Mbugua, Eugene Asike, Boniface Onyango, Eric Otieno na Ibrahim Joshua.