Matabibu kote nchini wametoa ilani ya mgomo ya siku saba wakidai makubaliano kadhaa ya awali ya kurejea kazini hayajatekelezwa.
Mwenyekiti wa chama cha matabibu nchini (KUCO) Peterson Wachira amesema mahakama iliamrusha kwa wajiri kufanya majadiliano kuhusu matakwa yao kabla ya kusitisha mgomo, lakini hadi wa leo masharti hayo hayajatimizwa.
Matabibu hao wamesema iwapo serikali haitatimiza matakwa yao kufikia Jumapili, usiku wa manane basi watalazimika kugoma.
Haya yanajiri huku mgomo wa waaguzi wakiingia siku ya 12 ya mgomo.