Masoud Pezeshkian amechaguliwa kuwa Rais mpya nchini Iran baada ya kumshinda mpinzani wake wa karibu Saeed Jalili katika duru ya pili ya uchaguzi.
Pezeshkian ambaye ni Daktari waupasuaji mwenye umri wa miaka 71, alijipata asilimia 53.3 ya kura zote zaidi ya milioni 30 zilizopigwa huku Jalili akipata asilimia 44.3.
Ilibidi upigaji kura kurudiwa baada kukosekana kwa mshindi wa moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya upgaji kura iliyoshohudia asilimia 40 pekee ya wapigaji kura waliojisajili wakishiriki Juni 28.
Uchaguzi huo uliitishwa kufuatia kifo cha Rais Ebrahim Raisi, aliyeuawa kwenye ajali ya ndege mwezi Mei mwaka huu.