Naibu Kamishna wa kaunti ya Tana River Andrew Mutua ametangaza kupiga marufuku natumizi ya mashua za kasi katika mto Tana, kufuakia mkasa wa kuzama kwa mashua Jumapili jioni eneo la Kona Punda.
Mutua ametangaza haya Jumatatu kufutia mkasa wa kuzama kwa mashua iliyokuwa na abiria 45 siku ya Jumapili.
Watu 22 walinusuriwa kwenye mkasa huo huku miili mitatu ikiopolewa, wakati wengi 22 wakiwa hawajulikani waliko.
Serikali imeapa kuwachukulia adhabu kali watakaokiuka matumizi ya mashua hizo za kasi katika mto Tana.