Mashua ndogo yazama Senegal, yawaua wahamiaji haramu 34

Vyombo vya kiuslama nchini Senegal Ijumaa iliyopita viliwakamata wahamiaji wengine haramu 142,  waliokuwa kwenye mashua wakielekea Uhispania.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mashua moja ndogo ilizamakaskazini magharibi mwa Senegal na kuwaua wahamiaji haramu 34 jana Jumapili. 

Mashua hiyo ilizama katika Bahari ya Atlantiki ikisafiri kutoka Afrika kuingia barani Ulaya.

Kulingana na vyombo vya kiusalama nchini Senegal, wahamiaji hao walikuwa wakielekea katika Visiwa vya Canary nchini Uhispania.

Eneo hilo la Bahari ya Atlantiki limesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 wanaojaribu kutorokea Ulaya kutoka Afrika.

Vyombo vya kiuslama nchini Senegal Ijumaa iliyopita viliwakamata wahamiaji wengine haramu 142,  waliokuwa kwenye mashua wakielekea Uhispania.

Wahamiaji hao haramu walijumuisha wanawake 23, na watoto wanne kutoka Senegal, Gambia, Guinea Bissau, Guinea na Nigeria.

Tayari miili 21 imeopolewa huku juhudi za kutafuta miili zaidi zikiendelea.

Watu wapatao 3,300 wameripotiwa kuwasili nchini Uhispania tangu mwanzoni mwa  mwezi huu kwa kutumia mashua zipatazo 30.

Share This Article