Mariga asema kutumiliwa kwake kulikuwa haramu

Mariga amekosoa mchakato huo akiutaja kuwa haramu na ambao haukufuata sheria wala katiba ya FKF.

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini, FKF aliyetimuliwa McDonald Mariga, amekashifu hatua ya kumbandua yeye pamoja na wanachama wengine sita wa kamati kuu madarakani Jumamosi iliyopita.

Mariga amekosoa mchakato huo akiutaja kuwa haramu na ambao haukufuata sheria wala katiba ya FKF.

Ameongeza kuwa mkutano huo maaluma ulioandaliwa kaunti ya Meru, ulilenga kuwanyamazisha wanachama hao saba wa NEC kudai uwazi na uwajibikaji katika FKF.

Aidha, Mariga amesema kuwa yeye na wenzake sita waliotimuliwa hawakupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kung’atuliwa inavyohitajika kwa mujibu wa katiba ya FKF.

Mchezaji huyo wa zamani wa Harambee stars na klabu ya Inter Milan ya Italia, amesema kuwa wajumbe wa mrengo wake 32 walinyimwa fursa ya kuingia ukumbini ili kupiga kura licha ya kuidhinishwa.

Share This Article