Rais William Ruto amesema kuwa serikali imesitisha kufadhili mashindano ya mbio za magari WRC na badala yake kuanzia mwaka ujao yatafadhiliwa na sekta za kibinafsi.
Rais alisema haya Jumapili katika hotuba ya kufunga rasmi makala ya mwaka huu ya mashindano hayo.
Aidha, Ruto alitaka kampuni za kibinafsi kushirkiana na kufanishikisha mashindano hayo.
Serikali imekuwa mfadhili mkuu wa mashindano tangu yarejeshwe kwenye kalenda ya dunia mwaka 2021.
Mazungumzo tayari yameanza na waandalizi wa WRC ili kuhakikisha mashindano hayo yatasalia kwenye ramani ya dunia.
Makala ya mwaka huu, yaliyoshindwa na dereva Katsuta Takamoto kutoka Japan, yalikuwa ya tano na kukamilisha mkataba wa kwanza kati ya serikali ya Kenya na shirika la kimataifa la mbio za magari FIA.