Makala ya 19 ya mashindano ya Riadha ya Dunia yalicheleweshwa kuanza kwa tarkiban lisaa limoja mapema Jumamosi kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha mjini Budapest Hungary.
Mvua hiyo ililazimika mashindano yote ya awamu ya asabuhi katika ratiba ya siku ya kwanza kusongezwa mbele kwa dakika 60 kwa kila shindano.
Wanariadha wapatao 2000 kutoka zaidi ya mataifa 200 watashindana katika fani 49 katika kipindi cha siku 9 za mashindano hayo.
Sherehe za ufunguzi zitaandaliwa kuanzia saa moja usiku majira ya Afrika Mashariki na mashindano hayo yanarushwa mubashara na runinga ya taifa KBC Channel 1.