Makala ya 11 ya mashindano ya mbio za magari ya East Africa Classic Safari Rally, yamepigwa jeki baada ya kupokea ufadhili wa shilingi milioni 6 kutoka kwa kampuni ya Safaricom.
Mashindano hayo yataanzishwa rasmi Jumamosi hii katika eneo la Vipingo na yamewavutia madereva 63 kutoka mataifa 27 duniani.
Mashindano hayo yatakamilika Disemba 18 na yatawashirikisha madereva 44 wa kimataifa na 19 wa humu nchini watakaoshindana umbali wa kilomita 4,000 katika kaunti 11 zikiwemo Kilifi, Nakuru na Nairobi.
Baadhi ya madereva wa humu nchini watakaoshiriki ni pamoja na bingwa mtetezi Baldev Singh Chager na bingwa wa zamani Kris Rosen.