Mashindano ya Doha Diamond yaahirishwa hadi Juni

Dismas Otuke
0 Min Read

Mkondo wa kwanza wa mashindano ya Diamond League mjini Doha yameahirishwa kutoka Mei 8 hadi Juni 19.

Aidha,mashindano hayo yamehamishwa kutoka uwanja wa Qatar Sports Club hadi ule wa Khalifa International.

Waandalizi wamesema wamelazimika kuahirisha mashindano hayo kutokana na joto jingi linaloshuhudiwa kwa sasa nchini humo.

Mashindano ya Diamond League  mwaka 2026,yataanzia kwa mkondo wa Bislet Games mjini Oslo,Noryway Juni 10.

Share This Article