Derby ya mashemeji kuwania alama za ligi kuu kati ya AFC Leopards na Gor Mahia, iliyokuwa ichezwe Jumapili hii imeahirishwa.
Kulingana na taarifa ya shirikisho la soka nchini FKF,mchuano huo umeahirishwa baada ya wenyeji Leopards kushindwa kupata uwanja.
Ni mara ya pili kwa mechi hiyo kuahirishwa baada ya mkondo wa kwanza kuahirishwa kutokana na ukosefu wa uwanja.