Mashabiki wa VIP pekee kuruhusiwa kupiga mtindi ndani ya uwanja Olimpiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Mashabiki wa jukwaa kuu VIP pekee ndio wataruhusiwa kunywa pombe ndani ya uwanja kwenye michezo ya Olimpiki, inayoendelea nchini Ufaransa.

Sheria za Ufaransa za mwaka 1991 zilipoiga marufuku uuzaaji wa pombe kwa mashabiki ndani ya viwanja wakati wa michezo isipokuwa tu wale wa jukwaa kuu.

Waandalizi wa Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu hawakushghulika kutaka kubadilishwa kwa sheria, hivyo basi pombe hairuhusi kuuzwa uwanjani katika makala ya 33 ya olimpiki yatakayokamilika Agosti 11.

Itakuwa mara ya pili mtawalia pombe kupigwa marufuku kuuzwa ndani ya viwanja vya michezo ya Olimpiki katika makala ya mwaka 2021 mjini Tokyo,Japan.

Pombe iliuzwa ndani ya viwanja vya Olimpiki katika makala ya mwaka 2012, jijini London Uingereza na Rio De Janeiro mwaka 2016.

Share This Article