Rais wa klabu ya soka ya Simba nchini Tanzania Mohammed Dewji maarufu kama “Mo Dewji” amewasihi mashabiki wa timu hiyo kusalia watulivu na kuwa na imani na viongozi wa timu hiyo ya mchezo wa soka.
Mashabiki hao wamekuwa wakilalamika kuhusu matokeo mabaya kwenye mechi yao ya mwisho dhidi ya mahasimu wao Yanga SC ambapo walishindwa mabao 5-1.
Dewji ambaye pia ni mfanyabiashara na mdhamini mkuu wa timu hiyo ameomba mashabiki hao kuendelea kufika uwanjani kushabikia timu hiyo kila inapocheza.
Mashabiki wanahisi kwamba ushinde huo ni wa aibu huku wakisema kwamba kushindwa kwa mabao matano sio shida ila wameshindwa na timu gani?
Wanataka viongozi wa timu hiyo wachukue hatua ya kuwasimamisha kazi maafisa husika kama ilivyofanyika kwa aliyekuwa kocha Robertinho.