Naibu Kamishna Mkuu wa Polisi Gilbert Masengeli hatimaye amejitokeza mahakamani Ijumaa, ili kujinusuru kifungo cha miezi sita gerezani alichohukumiwa wiki jana.
Masengeli amekula kiapo cha kujitetea katika kesi ya kupuuza mahakama mara tatu, alipoitwa kuelezea waliko wanaume watatu waliotekwa nyara mtaani Kitengela.
Naibu Kamishna huyo wa polisi alishtakiwa wakati akiwa kaimu Inspekta mkuu wa Polisi na kulingana na uamuzi wa Jaji wa mahakam kuu Lawrence Mugambi,Masengeli alihitajika kuanza kutumikia kifungu leo.
Hata hivyo wanaume hao watatu walitekwa nyara wamepatikana mapema Ijumaa ,lakini bado atalazimika kutumikia kifungo.