Maseneta wanaohudumu kwa muhula wa kwanza wamewabwaga vigogo katika mijadala na kuwasilisha hoja bungeni kulingana na utafiti wa kampuni ya Infotrak.
Utafiti huo unaonyesha kuwa maseta 16 wapya kati ya 39 waliochaguliwa kwa muhula wa kwanza, wamewashinda wale wanaohudumu kwa muhula wa pili au zaidi.
Seneta wa Busia na mpiganiaji wa haki Okiya Omutatah, ameorodheshwa bora kwa asilimia 59.
Kamau Murango ambaye ni Senata wa Muranga na mwenzake wa Kericho Aaron Cheruiyot,wanashikilia nafasi ya pili kwa kwa asilimia 56.
Seneta wa Makueni Dan Maanzo ni wa nne kwa asilimia 52, huku John Methu wa Nyandarua akikamilisha orodha ya tano bora kwa asilimia 51.
Utafiti huo ulifanywa kati ya Julai na Septemba mwaka huu katika kaunti zote 47.