Bunge la Seneti litasikiza na kuamua hatima ya Gavana wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza wiki ijayo.
Bunge hilo litasikiza pande zote mbili katika kesi hiyo Jumanne ijayo kabla ya kufanya uamuzi siku ya Jumatano.
Kulingana na kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Aaron Cheruiyot, kesi ya Gavana Mwangaza itasikizwa na kuamuliwa na bunge lote na wala sio kamati.
Gavana Mwangaza anawasilishwa katika bunge la Seneti kwa mara ya pili baada ya kunusuriwa na bunge hilo awali.
Gavana huyo anakabiliwa na makosa kadhaa ikiwemo matumizi mabaya ya afisi.