Marion Serenge atajwa mwanamichezo bora wa mwezi Juni

Tom Mathinji
1 Min Read
Marion Serenge.

Nyota wa soka Marion Serenge ametuzwa kwa kuwa mwanamichezo bora wa LG- SJAJ wa mwezi Juni, baada ya kuisaidia timu ya taifa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 kufuzu kwa kombe la dunia. 

Timu hiyo almaarufu, Junior Starlets, iliandikisha historia kwa kuwa timu ya kwanza ya soka ya Kenya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazoandaliwa katika Jamhuri ya Dominican.

Serenge aliisaidia Starlets kushinda mechi baina ya Ethiopia na Burundi huku ikijikatia tiketi ya fainali hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya LG kanda ya Afrika Mashariki Dongwon Lee, alielezea matumaini kuwa tuzo hiyo itampa motisha Serenge  kuendelea kuweka historia katika timu hiyo ya taifa katika ngazi za kimataifa.

“Tunajua Serenge atapata motisha kuongeza bidii zaidi, timu yake inapoiwakilisha Kenya katika michuano hiyo ya kimataifa,” alisema Lee.

Serenge alitwaa tuzo hiyo ya LG-SJAK,  baada ya kuwashinda wakinzani wengine wakiwamo Alexandra Ndolo wa shindano la Fencing na wenzake katika timu ya Starlets Velma Abwire na Elizabeth Ochoka.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *