Marijali wa Tanzania walipiza kisasi dhidi ya Kenya na kutwaa kombe la CECAFA

Dismas Otuke
1 Min Read

Kilimanjaro Stars  ya Tanzania ndio mabingwa wa kombe la CECAFA kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 baada ya kulipiza kisasi na kuishinda Rising Stars mabao 2-1 kwenye fainali ya Jumapili jijini Dares Salaam.

Kenya ilikuwa ya kwanza kufumania lango kunako dakika ya 48,baada ya kipindi cha kwanza kumalizikia sare tasa ,kabla ya Valentino Kusengama kukomboa kwa wenyeji Kilimanjaro  dakika ya 65.

Sekhani Khamis alipachika wavuni bao la ushindi kwa Kilimanjaro  katika dakika ya 82, huku wakilipiza kisasi cha kushindwa na Kenya magoli yayo hayo 2-1, katika mchuano wa kufungua mashindano kundini A .

Uganda Hippos walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuwacharaza Burundi mabao 3-1 mapema leo.

Tanzania na Kenya zimefuzu kuwakilisha ukanda wa CECAFA katika fainali za kombe la AFCON kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 mwaka ujao.

Website |  + posts
Share This Article