Marekani imetoa tahadhari ya usalama kwa raia wake wanaoishi nchini, kuhusu uwezekano wa kutekelezwa kwa mashabulizi ya kigaidi.
Kulingana na Ubalozi wa Marekani nchini Kenya mashambulizi hayo yanalenga maeneo yenye watu wengi na raia wa kigeni ,wakiwemo watalii wanaozuru jijini Nairobi na maeneo mengine nchini.
Ubalozi wa Marekani umewataka raia wake kuwa makini na waangalifu dhidi ya mashambulizi ya kigaidi na utekaji nyara.
Mashambulizi hayo ya kigaidi pia huenda yakalenga shule ,mikahwa,vituo vya polisi ,afisi za ubalozi ,maduka,masoko ma majumba ya kibiashara.
Wakenya na raia wa kigeni wameonywa kujienpusha na maeneo yenye umati na maandamano