Marekani imetaka kuachiliwa mara moja kwa Rais wa Niger Mohamed Bazoum aliyeshikwa mateka.
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken amekiri kuzungumza na Rais Bazoum anayekabiliwa na utata kufuatia jaribio la mapinduzi ya serikali.
Wanajeshi jana Jumatano walitangaza kuipindua serikali ya Rais Bazoum baada ya kuzingira na kumfungia kwenye ikulu na kuzuia watu wote waliokuwa katika ikulu kutoka au kuingia.