Marekani yampongeza Rais Ruto kwa kuchukua hatua za kupunguza machafuko

Dismas Otuke
1 Min Read
Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo na Rais William Ruto kufuatia maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024. 

Maandamano hayo yalisababisha vifo vya watu angalau 20 na mamia ya wengine kujeruhiwa.

Wakati wa mazungumzo yao yaliyofanywa kwa njia ya simu, Blinken alimpongeza Rais Ruto kwa kuchukua hatua za kupunguza machafuko na kuahidi kufanya mazungumzo na waandamanaji na mashirika ya kijamii.

Alimpongeza Ruto kwa kurejesha mswada huo tata wa fedha bungeni kama njia ya kupunguza machafuko.

Aidha, alikariri haja ya serikali na polisi kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji na kutaka uchunguzi ufanyike kuhusiana na ripoti za ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Blinken aliahidi kuwa Marekani itaendelea kushirikiana na serikali ya Kenya na watu wa Kenya katika jitihada za kukabiliana na changamoto za kiuchumi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *