Marekani yaitaka Rwanda kuondoa majeshi yake DRC

Dismas Otuke
1 Min Read

Marekani imeitaka Rwanda kusitisha kusaidia kundi la waasi wa M23, linalopigana katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Msemaji wa ikulu ya nchi hiyo, Tammy Bruce, ameitaka serikali ya Rwanda kuondoa majeshi yake yote nchini DRC.

Kwenye taarifa yake, Bruce ameitaka Rwanda kuheshimu uhuru wa DRC.

Aidha, amezitaka nchi za Rwanda na DRC kuwashtaki wahusika wote wa utwaaji wa miji ya Goma na Bukavu na ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *