Marekani wameanza vyema harakati za kutetea kombe la dunia kwa wanawake kwa ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya limbukeni Vietnam, katika mchuano wa kundi E uliosakatwa kiwarani Edenpark mjini Auckland Newzealand mapama Jumamosi.
Sophia Smith alipachika bao la kwanza kunako dakika ya 14 na kuongeza la pili dakika ya 47 Wamarekani wakienda mapumzikoni kwa uongozi wa magoli mawili kwa sufuri.

Lindsey Hoaran alikongomelea msumari wa mwisho katika jeneza la Haiti kwa goli la tatu dakika ya 77 akisaidiwa na Smith.
Marekani walishinda kombe la dunia kwa mara ya pili mtawalia mwaka 2019, na wanawania kuweka historia kwa kutwaa mara tatu kwa mpigo, kwenye fainali za mwaka huu zinazoandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Newzealand na Australia.