Marekani na Iran zafikia makubaliano ya kusitisha vita

Makubaliano kati ya nchi hizo mbili yatasainiwa rasmi wakati wa hafla itakayoandaliwa nchini uswizi Ijumaa wiki hii.

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya Anadolu Ajansı

Hatimnaye nchi za Marekani na Iran zimefikia makubaliano ya kusitisha vita ambavyo vimedumu kwa kipindi cha miezi mitatu na nusu. 

Marekani na Israel zilianzisha vita dhidi ya Iran Februari 28 mwaka huu.

Pakistan, kupitia Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, ambayo imekuwa mpatanishi wa mzozo kati ya nchi hizo mbili imedokeza kuwa mkataba rasmi wa kusitisha vita hivyo utatiwa saini Ijumaa wiki hii.

Kupitia mitandao ya kijamii jana Jumapili, Rais wa Marekani Donald Trump aliashiria kuwa “Makubaliano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa yamekamilika.”

“Na sasa ninaidhinisha kikamilifu kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz bila malipo, na sambamba na hilo, ninaidhinisha kuondolewa mara moja kwa kizuizi cha Jeshi la Wanamaji la Marekani,” alisema Trump kwenye ujumbe wake.

“Meli za Dunia, washeni injini zenu. Wacheni mafuta yatiririke.”

Makubaliano hayo yatatiwa saini rasmi wakati wa hafla itakayoandaliwa nchini Uswizi.

 

 

 

 

Share This Article