Marekani kumenyana na Korea nusu fainali Kombe la Dunia kwa mabanati

Dismas Otuke
1 Min Read

Marekani itamenyana na Korea Kaskazini katika nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 katika Jamhuri ya Dominica.

Marekani ilitinga semi fainali baada ya kuwabandua waakilishi pekee wa Afrika waliosalia mashindanoni Nigeria mabao mawili kwa bila wakati Korea Kaskazini ikiwalaza Poland bao moja kwa bila katika robo fainali.

Uhispania itakabiliana na Ecuador nao Japan wapimane ubabe na Uingereza katika kwota fainali mbili za mwisho Jumapili usiku na mapema Jumatatu mtawalia.

 

Share This Article